WIZARA YA UTALII NA MAMBO YA KALE
USHIRIKI WA MKUTANO WA KILELE CHA Z-SUMMIT
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Nd. Fatma Mabrouk Khamis akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh. Mudrik Ramadhan Soraga katika kilele cha Mkutano wa Z-Summit uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Nellan uliopo Shangani Mjini Zanzibar.
Zanzibar yaadhimisha siku ya Utalii Duniani
Makamo wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Othman Masoud Othman ashiriki Kongamano la Siku ya Utalii Duniani lililoandaliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale

Search Engine Optimization

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Link Building Service

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Creative Campaigns

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Email Marketing Solution

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Ifahamu Taasisi Yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa mwaka 2020, kwa mujibu wa uwezo aliopewa Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu 42 (1) cha Katiba ya mwaka 1984, na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Utalii na Mambo ya Kale.

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa kutokana na shughuli zake kufanana na kutegemeana katika utendaji wa kazi. Hivyo, kuziweka katika Wizara moja shughuli hizo kutasaidia kupatikana ufanisi, kusukuma kasi ya maendeleo na kuimarisha uchumi.

Wizara inashughulikia Sekta kuu mbili (2) za Utalii na Mambo ya Kale. Sekta ya Utalii inajumuisha Kamisheni ya Utalii na Idara ya Utalii. Taasisi hizi zimekabidhiwa jukumu la kupanga, kusimamia, kuendeleza Utalii na kuitangaza Zanzibar kama ni kivutio cha utalii ili kwenda sambamba na sera, mikakati na Dira ya Taifa katika kufikia malengo makuu ya kuimarisha uchumi na kupunguza umasikini.

Kwa upande wa Mambo ya Kale, Sekta inaundwa na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale. Sekta hii imekabidhiwa jukumu la kuhifadhi, kuimarisha na kutunza maeneo na vitu vya kale na kihistoria ili visaidie katika kuimarisha uchumi na kutunza historia kwa vizazi vijavyo.

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz