Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa mwaka 2020, kwa mujibu wa uwezo aliopewa Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu 42 (1) cha Katiba ya mwaka 1984, na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Utalii na Mambo ya Kale.

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa kutokana na shughuli zake kufanana na kutegemeana katika utendaji wa kazi. Hivyo, kuziweka katika Wizara moja shughuli hizo kutasaidia kupatikana ufanisi, kusukuma kasi ya maendeleo na kuimarisha uchumi.

Wizara inashughulikia Sekta kuu mbili (2) za Utalii na Mambo ya Kale. Sekta ya Utalii inajumuisha Kamisheni ya Utalii na Idara ya Utalii. Taasisi hizi zimekabidhiwa jukumu la kupanga, kusimamia, kuendeleza Utalii na kuitangaza Zanzibar kama ni kivutio cha utalii ili kwenda sambamba na sera, mikakati na Dira ya Taifa katika kufikia malengo makuu ya kuimarisha uchumi na kupunguza umasikini.

Kwa upande wa Mambo ya Kale, Sekta inaundwa na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale. Sekta hii imekabidhiwa jukumu la kuhifadhi, kuimarisha na kutunza maeneo na vitu vya kale na kihistoria ili visaidie katika kuimarisha uchumi na kutunza historia kwa vizazi vijavyo.

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz