Majukumu ya Ofisi Kuu Pemba
Ofisi Kuu Pemba imeanzishwa kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Utawala, Uendeshaji na Mipango Mikuu ya Wizara kwa upande wa Pemba. Kiongozi mkuu wa Ofisi Kuu Pemba ni Afisa Mdhamini ambae anateuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Ofisi Kuu Pemba imegawika katika divisheni (4) ambazo ni Utumishi, Mipango, Utalii na Makumbusho na Mambo ya Kale na vitengo vitano ambavyo ni Uhasibu, Ukaguzi wa Ndani, Uhusiano, TEHAMA na Manunuzi
Muundo wa Ofisi Kuu Pemba.