MAJUKUMU YA WIZARA.
Wizara ya Utalii, na Mambo ya Kale ina Majukumu makuu yafuatayo: -
- Kusimamia na kuendeleza Utalii kwa lengo la kuinua pato la Taifa na uchumi wa wananchi;
- Kutangaza utalii ndani na nje ya nchi;
- Kuhifadhi, kulinda na kuendeleza maeneo yote ya kihistoria nchini;
- Kukusanya mapato ya huduma zinazotolewa katika Maeneo ya Kihistoria na Kamisheni ya Utalii;
- Kuratibu uibuaji wa miradi, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia sekta ya Utalii na Mambo ya Kale;
- Kuandaa Sera, Sheria na mikakati ya kuendeleza sekta ya Utalii na Mambo ya Kale pamoja na kusimamia utekelezaji wake.