IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

Majukumu ya Idara ya Uendeshaji na Utumishi

Idara ya Uendeshaji na Utumishi ina jukumu la kusimamia shughuli za Uendeshaji na Utumishi zikiwemo kusimamia Sheria, Kanuni na miongozo ya Utumishi wa Umma kwa wafanyakazi.

Majukumu Mahsusi ya Idara ya Uendeshaji na Utumishi ni: -

 1. Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa Mpango wa Rasilimali Watu;
 2. Kuandaa na kusimamia mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi wa Wizara;
 3. Kusimamia mawasiliano na mashirikiano kati ya Wizara na Taasisi zake;
 4. Kusimamia maslahi ya watumishi, nidhamu na uwajibikaji.

 

 

Muundo wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi

Idara ya Uendeshaji na Utumishi imegawika katika Vitengo tatu (3), ambazo ni Utumishi, Uendeshaji na Utunzaji wa Kumbukumbu.

Kitengo cha Uendeshaji.

Majukumu

 1. Kutoa huduma za Utawala kwa Wizara husika
 2. Kusaidia nidhamu ya wafanyakazi.
 3. Kuainisha matatizo ya wafanyakazi.
 4. Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya Wizara ikiwemo usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano.
 5. Kusimamia majengo na mali nyengine zisizohamishika.
 6. Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Wizara.

Kitengo cha Utumishi

Majukumu

 1. Kutoa huduma za uongozi Rasimali Watu kwa Wizara husika.
 2. Kutunza kumbukumbu sahihi wafanyakazi.
 3. Kutayarisha Bajeti ya mafunzo ya Wizara.
 4. Kusimamia nidhamu, taratibu, kanuni na sheria za kazi.
 5. Kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya watumishi.
 6. Kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
 7. Kuwaelimisha watumishi kuhusu mipango ya mafunzo kwa mujibu wa kada zao.
 8. Kutoa mafunzo pahali pa kazi (on the job training) kwa maafisa Utumishi daraja la II walioajiriwa kwa mara ya kwanza.
 9. Kukusanya, kuchambua, kuhakiki na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.

 

Kitengo cha Utunzaji Kumbukumbu.

Majukumu

 1. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
 2. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
 3. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
 4. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki. (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbuukumbu.
 5. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
 6. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasis za Serikali

 

 

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz