IDARA YA MAKUMBUSHO NA MAMBO YA KALE

Majukumu ya Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale

Idara hii imeundwa mwaka 2010 mara baada ya kumalizika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2010 na inaongozwa na Mkurugenzi ambaye huteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa sharia iliyowekwa inayojulikana kama “The Ancient Monument Preservation Act No. 11 of 2002” inayotokana na marekebisho ya sheria ya mwaka 1927 (Link ya sheria).

Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale imeanzishwa kwa lengo la kuhifadhi, kuyalinda na kuyaendeleza majengo na maeneo ya kihistoria ya Unguja na Pemba.

Majukumu Mahsusi ya Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale.

  1. Kuhifadhi, kulinda na kuendeleza majengo na maeneo ya kihistoria ya Unguja na Pemba,
  2. Kuendesha tafiti za kihistoria na Akiolojia;
  3. Kuvumbua na kuyatambua maeneo mapya ya kihistoria;
  4. Kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kutunza historia ya nchi;
  5. Kuhifadhi kumbukumbu za historia na utamaduni wa Zanzibar kwa njia ya maonesho “dissemination”;
  6. Kutangaza maeneo ya kihistoria na makumbusho ndani na nje ya Zanzibar;
  7. Kusimamia sheria na sera za Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale;
  8. Kuhakikisha rasilimali za historia na urithi wa utamaduni zinatumiwa ipasavyo;
  9. Kushirikiana na taasisi nyengine za kitaifa na kimataifa katika nyanja mbalimbali za urithi wa utamaduni.

Muundo wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale

Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale imegawika katika divisheni tatu ambazo ni Makumbusho, Mambo ya Kale na Utawala.

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz