MALENGO YA WIZARA

Lengo kuu la Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ni kuratibu na kutangaza utalii, kulinda na kuhifadhi maeneo ya kihistoria. Lengo hili litasimamiwa kupitia sera, sheria, kanuni na miongozo inayohusiana na Sekta ya Utalii na Mambo ya Kale.

  1. Kuendeleza na kukuza maendeleo na Sera ya Utalii ili kuongeza kwa kiasi kikubwa mchango wa Utalii kweye pato la Taifa, ajira na fedha za kigeni.
  2. Kuongeza tija ya sekta ya Utalii na kuweka mazingira na rasilimali watu bora katika uandaji, utekelezaji na usimamizi wa sera na mipango ya Utalii.
  3. Kuwa na maeneo ya kihistoria yaliyoimarika na yenye ubora wa viwango vya Kitaifa na Kimataifa.
  4. Kuongeza uelewa kwa wakazi wa Tanzania na jamii ya kimataifa kuhusu bidhaa na huduma za Utalii zilizopo Zanzibar.
  5. Kusimamia na kuendesha vizuri wa rasilimali watu katika Wizara.
  6. Kusimamia na kuratibu mipango mikuu, Sera na Tafiti za Wizara.

 

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz