Wizara ya Utalii yawasilisha ripoti
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Simai Mohammed Said akiwasilisha ripoti ya utekelezaji kwa Kamati ya Biashara, Utalii na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi
PUMZIKENI KWA AMANI
Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar inaungana na watanzania wote katika wakati huu mgumu wa msiba uliotokana na ajali ya ndege ya shirika la ndege la Precision Air
Waziri Simai ashiriki usafi Prison Island
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said akishiriki katika zoezi la usafi katika kisiwa cha Changuu(Prison Island) leo 05/11/2022 ambapo limewashirikisha pia Chama cha Wafanya Mazoezi Zanzibar(ZABESA)
Vuta Nkuvute yazidi kupasua anga
Filamu ya Vuta Nkuvute iliyomshirikisha msanii Siti Amina ambae ni Balozi wa Utalii kwa upande wa sanaa na muziki imejishindia tuzo 4 kati ya 14 iliyoshindania kwa kupitia jukwaa kubwa la filamu Afrika la Africa Movie Academy Awards 2022
Zanzibar yaadhimisha siku ya Utalii Duniani
Makamo wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Othman Masoud Othman ashiriki Kongamano la Siku ya Utalii Duniani lililoandaliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
UFUNGUZI WA KASRI YA KIBWENI
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mheshimiwa Simai Mohammed Said akifungua rasmi makumbusho ya Kasri ya Saada iliyopo Kibweni,Mkoa wa Mjini Maghribi tarehe 16/03/2022.
MAKABIDHIANO
Aliekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mheshimiwa Lela Muhamed Mussa akimkabidhi majukumu waziri mpya wa wizara hiyo Mheshimiwa Simai Mohammed Said katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Wizara hiyo uliopo manzimoja tarhe 14/03/2022
ZIARA YA MHE. WAZIRI KISIWANI PEMBA
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mheshimiwa Simai Mohammed Said ameendelea na ziara yake kisiwani Pemba , ambapo ametembelea maeneo mbalimbali ya Vivutio na kihistoria ikiwemo Makangale,Msitu wa Ngezi na Chwaka Tumbe.
MHE. WAZIRI AKISHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA USHIRIKIANO BAINA YA ZATI NA EXIM BANK
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mheshimiwa Simai Mohammed Said ameshuhudia utiaji saini mkataba wa ushirikiano baina ya ZATI (Zanzibar Association of Tourism Investors) na Exim Bank iliyofanyika tarehe 25/03/2022 katika hoteli ya Park Hyatt.

Ifahamu Taasisi Yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa mwaka 2020, kwa mujibu wa uwezo aliopewa Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu 42 (1) cha Katiba ya mwaka 1984, na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia na kuendeleza Sekta za Utalii na Mambo ya Kale.

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeanzishwa kutokana na shughuli zake kufanana na kutegemeana katika utendaji wa kazi. Hivyo, kuziweka katika Wizara moja shughuli hizo kutasaidia kupatikana ufanisi, kusukuma kasi ya maendeleo na kuimarisha uchumi.

Wizara inashughulikia Sekta kuu mbili (2) za Utalii na Mambo ya Kale. Sekta ya Utalii inajumuisha Kamisheni ya Utalii na Idara ya Utalii. Taasisi hizi zimekabidhiwa jukumu la kupanga, kusimamia, kuendeleza Utalii na kuitangaza Zanzibar kama ni kivutio cha utalii ili kwenda sambamba na sera, mikakati na Dira ya Taifa katika kufikia malengo makuu ya kuimarisha uchumi na kupunguza umasikini.

Kwa upande wa Mambo ya Kale, Sekta inaundwa na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale. Sekta hii imekabidhiwa jukumu la kuhifadhi, kuimarisha na kutunza maeneo na vitu vya kale na kihistoria ili visaidie katika kuimarisha uchumi na kutunza historia kwa vizazi vijavyo.

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz