IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

Majukumu ya Idara ya Mipango, Sera na Utafiti

Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ina majukumu ya kupanga, kuratibu na kusimamia mipango, sera na tafiti za Wizara

Majukumu Mahsusi ya Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni: -

  1. Kuandaa na kusimamia miradi ya maendeleo ya Wizara;
  2. Kuandaa bajeti ya Wizara na kusimamia utekelezaji wake;
  3. Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya programu na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Wizara;
  4. Kutayarisha na kuzifanyia mapitio sera za Wizara
  5. Kuratibu tafiti mbalimbali za Wizara.

Muundo wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti

Muundo wa Idara ya Mipango Sera na Utafiti umegawika katika Vitengo vitano (5) ambavyo ni Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini, Maendeleo ya Sera, Utafiti na Mipango ya Kisekta.

Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini.

Majukumu.

  1. Kuandaa viashiria vya taarifa ya ufuatiliaji kwa kuzingatia mahitaji ya Mpango Mkuu wa ufuatiliaji wa Mkuza.
  2. Kutayarisha mfumo wa muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripoti za utekeklezaji.
  3. Kuandaa na kushiriki katika ziara za ufuatiliaji na tathmini zinazofanyika na kuhakikisha zinafuata mifumo iliyokubalika katika ukusanyaji wa taarifa.
  4. Kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwemo kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini wa ndani ya Wizara.
  5. Kukusanya taarifa za uchambuzi wa takwimu zinazohitajika katika kutayarisha Sera, Mipango pamoja mapendekezo ya bajeti.

 

Kitengo cha Maendeleo ya Sera

Majukumu.

  1. Kutayarisha Sera zinazohitajika na kushauri kwa uongozi.
  2. Kuzichambua Sera zilizopo za Wizara kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya utekelezaji.
  3. Kufanya uchambuzi juu ya masuala ya uchumi, kijamii na kiutawala na kuishauri Wizara kutayarisha Sera zinazohitajika.
  4. Kuwasilisha na kufanya kazi pamoja na Tume ya Mipango kwa kutayarisha na kutekeleza Sera mpya ili kuhakikisha kuwa zinakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango ya kitaifa.

 

Kitengo cha Utafiti

Majukumu.

  1. Kufanya tafiti na chambuzi za utekelezaji wa Mipango, Miradi na Programu mbali mbali zinazotekelezwa na Wizara na kutayarisha maelezo ya kisekta.
  2. Kufanya uchambuzi juu ya namna ya utoaji wa huduma na kukusanya mawazo/maoni kwa wadau juu ya huduma zinazotolewa na Wizara.
  3. Kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu katika kufanya tafiti na uchunguzi unaohusiana na majukumu ya Wizara na kusaidia kazi za Idara a Uchumi na Maendeleo katika kutekeleza majukumu yao.

 

Kitengo cha Mipango ya Kisekta na Maendeleo.

Majukumu

  1. Kukusanya taarifa za Mpango Kazi wa mwaka na Mpango Mkakati wa muda wa kati wa Wizara.
  2. Kuwasiliana na kufanya kazi pamoja na Tume ya Mipango wakati wa kutayarisha mipango mipya ili kuhakikisha inakwenda sambamba na utekelezajiwa Wizara.
  3. Kukusanya taarifa za program/miradi ya Wizara na Mipango Kazi.
  4. Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa bajeti ya Wizara.
  5. Kushirikiana na sekta binafsi katika mambo mbali mbali ya Wizara.
  6. Kufanya utafiti na kubainisha fursa katika sekta husika.

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz